Swahili


MFUPA YA ISHANGO
MFUPA ULIOSIMIKWA PA ISHANGO UNAAMANISHI NINI ?

Kati ya milioni ya vyombo vilivyo tambuliwa na timu la bwana Jean de Heinzelin pa Ishango, kuna vyenye kustusha kuliko vingine. Kwa namna ya upekee, kuna chombo kimoja kilichovuta mawazo yake na kuwa chanzo cha mafunzo ya historia ya Africa, yaani : MFUPA ULIOSIMIKWA PA ISHANGO.

Kulingana na mila, uitwa « fimbo ya Ishango ». Ni chombo yenye kuchongoka inayounganishwa na kopo pamoja na mti wa mfupa. Kwa hiyo, chombo hicho ni cha upekee pamoja na vingine vilivyolindwa kwa utafiti wa historia, kwani kwa kawaida havizowee kupatikana. Kopo hiyo iliyo laini yenye kupatikana huko pembeni, ilisaidia kwa kuhakikisha kazi iliyo fanyika, kama vile kwa mfano kuchanja mwili (yaani ngozi).

Mfupa unaopatikana kwenye mti, ulipaliliwa, kwa ginsi si kwepesi kutambua vizuri asili yake. Hakika, ilikuwa myama anayekuwa na maziwa kifuani mwake.

Sasa, ni jambo gani linalo stusha ?
Ni mti wa chombo hicho uliyo tambulisha mfupa huo, kwani mapambo yake yazaa na kuendelea kuzaa maulizo mengi kuhusu samani yake kamili. Mti huo una vipimo sehemu kwa ndondogo mia moja na makumi sita na mnane kwa ngambo mbili. Vipimo hivyo vidogo vidogo vinakusanywa ngambo mbili yenye kugawanywa kwa nguzo tatu yenye kupatikana pembeni ya fimbo.

Wazo lenye kutarajiwa
Bwana Jean de Heinzelin alifikiria ya kwamba alama hizo ziliamanisha tarakimu. Ilitambulikana wazi kama kwa nyakati za historia, hesabu huandikwa kwa alama. Tangu hapo, bwana de Heinzelin alitafuta kupata kitu chenye kuweza kulinganishwa na hesabu, ambacho uweza kupatikana kati ya tarakimu hizo, pia kutambua uhusiano pamoja na mafunzo ya hesabu yenye kuendelea zaidi na isiyo julikana hadi sasa, hata kwa wakati wa zamani.
Hii ni mafikiri ya bwana Jean de Heinzelin aliyoandika katika kitabu chake mnamo mwaka 1957 kuhusu kituo cha Ishango.

Nguzo la kati
Nguzo hilo laonyesha tarakimu moja ikijumlishwa mara mbili ; kama vile tatu na sita ; inne na mnane ; tano na kumi. Kwa hiyo, kuna tarakimu mbili zisizo fasiriwa ; yaani tano na saba.

Nguzo la kuume
Kwa upande huu, tarakimu zina uhusiano na tarakimu kumi, iliyo msinji unaojulikana vizuri.
Kwa hiyo tuseme hivi :

  • Kumi na moja ; inaamanisaha kumi kuongeza moja : 11 = 10 + 1
  • Makumi mbili na moja ; inaamanisha makumi mbili kuongeza : 21 = 20 + 1
  • Moja : Kumi na kenda ; inaamanisha makumi mbili kutosha moja : 19 = 20 - 1
  • Kenda ; inaamanisha kumi kutosha moja : 9 = 10 - 1


Nguzo la kushoto
Wakaaji wa Ishango walitambua tarakimu hizo za kwanza yaani kumi na moja, kumi na tatu, kumi na saba, pia saba na kumi na kenda. Ndizo tarakimu za kwanza zenye kupatikana kati ya kumi na makumi mbili. Tarakimu la kwanza ni lenye kugawanywa peke yake.

Watafiti wengine walijiusisha na mafasirio ya sehemu hizo.
Wataalamu wa hesabu ; kama vile Dirk Huylerbrouck na Vladmir Pletser walichukua mawazo yenye bwana Jean de Heinzelin aliotoa hapo mwanzo na kutengeneza fimbo kama vile kanuni kwa kufanya hesabu, kulingana na misinji ya tarakimu tatu na inne, na kwa kuelekea juu zaidi, kupata msinji wa tarakimu kumi na mbili, yaani tatu mara inne (kujumlisha). Kwa upande ungine, wanatambua kama hakuna hakikisho kamili kuhusu ujuzi wa tarakimu hizo za kwanza.

Kwa upande wake, bwana Alexande Marshack, aliye mtaalamu wa mafunzo ya historia kwenye chuo kikuu cha Harvard, anafikiria pia namna ya kuandika tarakimu, ila kwa uhusiano na mwendo wa mwezi.

Bwana Olivier Keller, aliye pia mtaalamu wa mafunzo ya hesabu, anaharifu kuhusu hatari ya kizazi cha sasa kutazama tarakimu mahali kote. Kwake yeye, tabia hiyo inaweza kumzuwia mtaalamu yeyote kutambua alama zingine zenye kupatikana katika vitu vingine ; kama vile : mfupa, jiwe, ao vyombo vya usanii vyenye kustahili kutiwa pia mkazo.

Jambo lenye kustusha ? Tukumbuka kama jambo hilo linaeneza sasa miaka elfu makumi mbili na tano…

Ikiwa siku moja mawazo kuhusu mafunzo ya hesabu inahakikishwa, itaamanisha kama watu wa wakati wa kale ; yaani «paléolithique» walikuwa na ujuzi wa hali ya juu kuhusu mafunzo ya hesabu.

Kwa hiyo, maulizo mengi yataulizwa. Walitumia vyombo hivyo kwa nia gani ? Kwa nini waliweka alama/misinji mingi ya hesabu ? Waliweza kugawa ujuzi huo kwa watu wote ? mafunzo hayo inayo faida kwa wavuvi ?

Kwa siku hizi za leo, kituo cha Ishango hakikuweza kutoa siri yake yote. Kwa upande ungine, ndani ya bonde la Semliki, upatikana pia vituo vingine vya mafunzo ya historia. Jimbo hilo la Afrika iliweza kuwapokea watu wa aina «Homo sapiens sapiens» tangu yapata myaka elfu mia moja.

Hadi sasa, tunakosa vifaa vingi kwa kufamu vizuri hali ya maisha pia mawazo ya wakaaji wa Ishango. Kwa hiyo, siku moja, itawaomba wataamalu wa arkelojia kurudi upande wa ziwa Edouard kwa kukamilisha kazi walio anza tangu mwaka 1950.

Tunayo matumaini kama kuna vifaa vya lazima vyenye kufichwa hadi sasa.

Kazi hii imetayarishwa na « Association pour la Diffusion de l’Information Archéologique » ;
Institut Royal des Sciences Naturelles de Belgique


  • Traduit par Augustin NDIMUBANZI BAZIRAKE domicilié à GOMA-RDC - Directeur en charge du Développement du Registre Numérique des citoyens des villes du Nord-Kivu-Licencié en Développement Rural, option : Environnement et Développement durable, Gradué en Pédagogie Appliquée, option : Français et Linguistique Africaine - CEO de la Fondation ISHANGO MILELE en RDC - traduction supervisée par MWANA SOLEIL A.S.B.L.

Créez votre propre site internet avec Webador